Assalam aleykum ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa machapisho yetu katika Blog yetu ya Blue magazine na hatimae leo tumekutana tena katika makala nyingine inayohusu utengenezaji wa mafuta ya mgando. ungana nami hatua kwa hatua mpaka mwisho wa makala hii na natumai utajifunza mengi.
Utengenezaji wa mafuta ya mgando
-Mahitaji
1-Micro wax
2-pafyumu
3-White oil
4-Rangi
Matengenezo
1-Chukua micro wax kilo moja (kg 1) na uweke ndani ya sufuria kisha injika kwenye moto
2-Subiri micro wax ipate moto na hatimaye iyeyuke kabisa
3-Chukua White Oil Lita 2 mimina ndani ya sufuria na uhakikishe Ime changanyikana kabisa
4-Weka rangi yako katika mafuta yako (kama utapenda kijiko kimoja)
5-weka pafyumu ili kuyafanya mafuta yako yanukie manukato
6-Acha yaanze kupoa mpaka yawe mazito
***Na hapo mafuta yako yatakuwa tayari unaweza kuyatumia katika kupaka mwilini au kufunga kwenye vifungashio na kwenda kuuza.*****
Mpaka hapo tunasema hatuna la ziada katika makala hii na tunakushukuru wewe kwa kufutilia makala hii kama utakuwa na Maswali,maoni,ushauri,au nyongeza unaweza tuandikia hapo chini. Asante kwa kufuatilia makala za Blue magazine